JINSI YA KUTENGENEZA MISHUMAA BORA IMARA

Ni rahisi sana kutengeneza mshumaa!



Mshumaa unatengenezwa katika maumbo mbali mbali kama wewe tu unavyopenda, pia na rangi...

Mishumaa inaweza kuwa ya:

1.kuweka chooni kupunguza harufu na kuleta mandhari nzuri (Hapa kuna kemikali inayochanganywa kwa ajili ya kupunguza harufu, kuna perfume yake maalum)

2. Kuweka chumbani kwako kwa ajili ya matumizi yako na mwandani wako kama unae. Hapa napo kuna mchanganyiko wake unaotakiwa.



3. Mishumaa mingine ipo kwa ajili ya mapambo katika maeneo maalum kama KANISANI, SEBULENI na mishumaa vile vile inaweza tumika msibani.. matumizi yanatofautiana tu kulingana na mahitaji....

Kama nilivyozungumzia suala la rangi ya mshumaa, umbo na eneo unalotakia kutumia, hivi vitu ni muhimu sana kutambua ili ujue mshumaa wako uutengeneze katika umbo la aina gani.



Kuna mishumaa ambayo ni kwa ajili ya luxury tu ndo maana tunaona inakuja na maumbo ya kupendeza na kuvutia sana! Hiyo ni gharama kubwa kui design na kuifikisha sokoni kwa mlaji...

Mishumaa ambayo inaenda kwa mlaji (consumer) ambayo ni ile midogo midogo myeupe, ni rahisi sana kuitengeneza kwa sababu haihitaji mambo mengi....

NB: Mshumaa unaweza kuutengeneza hata kwa dakika 10 tu ukiwa mtaalam hasa! Ni jambo tu la kucheza na kemikali na kama una malighafi zote zinazohitajika.






*JINSI YA KUTENGENEZA MISHUMAA*



*Malighafi na Vifaa*


● Mafuta ya taa waxi/ Nta (Paraffin wax)
● Asidi boriki na Stearine
● Rangi (ukipenda)
● Pafyumu (ukipenda)
● Utambi / uzi
● Umbo (mould) ya mshumaa
● Jiko la mafuta ya taa/ mkaa na sufuria na ● vijiko vya chakula
● Vifungashio vyenye lebo



*Utengenezaji*


Utambi
Changanya asidi boriki vijiko 5 vya chakula na maji vijiko 4 vya chakula
Koroga kwa dakika 5
Tumbukiza utambi ukae kwa dakika 5
Anika ukauke
Mshumaa
Andaa maumbo ya mshumaa




Weka utambi katikati ya chombo kwa kushikiza na ute wa mshumaa na funga utambi
Weka sufuria jikoni, changanya nta kilo 1, stearine vijiko 4, chemsha  
Changanya rangi, parfyumu, asidi na koroga hadi mchanganyiko uyeyuke



Epua, mimina mchanganyiko kwenye maumbo na weka kwenye kivuli hadi mchanganyiko unaganda
Ondoa mshumaa taratibu kutoka kwenye maumbo

*Vifungashio na lebo*


Fungasha mishumaa kwenye chombo kitakachomvutia mteja aweze kununua



Bandika lebo kwenye chombo kuhusu bidhaa: Aina, mchanganyiko wa malighafi, uzito au idadi, maelekezo ya matumizi na uhifadhi, jina na anwani ya mtengenezaji, namba ya simu na barua pepe
....

Endelea kuwa nasi hapa hapa!《 Ng'e Amazing TV 》 kwa elimu mbalimbali kama hii


..
#ngeamazing #ngeamazingTV #JinsiyaKutengenezaMishumaa #DalasaLeo

..i usisahau kwenda YouTube Ch

USISAHAU KWENDA YOUTUBE 《 Ng'e Amazing TV 》CHANNEL YETU,, ,,, KISHA BONYEZA NENO SSUBSCRIBE ,, ,,,,, ,,,ILI USIPITWE NA ELIMU KAMA HIZI ..



Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog

AUDIO | Dogo Chande - MAMA