JINSI YA KUPIKA SAMBUSA TAMU ZA VIAZI
Jinsi Ya Kupika Sambusa za Viazi Sambusa za viazi ni kitafunwa kitamu, nafuu, na rahisi kupika. Zinaweza kuliwa wakati wa kifungua kinywa, futari, au kama vitafunwa vya chai. Ladha yake ni tamu na yenye viungo vya asili vinavyoleta harufu nzuri. Katika makala hii nitakuelekeza jinsi ya kupika sambusa za viazi hatua kwa hatua. Viungo: Kwa Kujaza Sambusa (Filling) ● Viazi – 4 vikubwa (vilivyochemshwa na kusagwa) ● Kitunguu maji – 1 kikubwa (kimekatwa vidogo) ● Kitunguu saumu na tangawizi – Vijiko 2 vya chakula (vimesagwa) ● Pilipili manga – Nusu kijiko cha chai ● Chumvi – Kijiko 1 cha chai ● Pilipili hoho – 1 (imekatwa vidogo) ● Mchanganiko wa bizari (curry powder) – Kijiko 1 cha chai ● Giligilani (coriander) – Kiasi kidogo (chopped) ● Mafuta ya kupikia – Vijiko 2 vya chakula Kwa Ganda la Sambusa (Samosa Wrappers): ● Unga wa ngano – 2 vikombe ● Chumvi – Nusu kijiko cha chai ● Maji – Kiasi kinachotosha ● Mafuta – Vijiko 2 vya chakula Hatua za Kupika Sambusa za Viazi 1. Kutayarisha Mc...