(UFUNUO) MOYO WA JIWE
UFUNUO: MOYO WA JIWE* facebook :- (Ng'e Amazing Gospel) *EZEKIELI 36:26* _“Nami nitawapa ninyi moyo mpya, nami nitatia roho mpya ndani yenu, nami nitatoa moyo wa jiwe uliomo ndani ya mwili wenu, nami nitawapa moyo wa nyama.”_ Swali je kwa mkristu katika Yesu tuna moyo wa jiwe au moyo wa nyama, Jibu swali hili kwanza kwa hoja ya maandiko kisha weka notes zako pembeni sasa tuamze *MOYO לב Lamed na Bet* - *ל Lamed* fimbo ya mwalimu, kuinua, kunyanyua. Inaonyesha moyo ni kitu kinachoinuliwa kutoka chini, kinachoongozwa juu kuelekea mlango wa uzima. - *ב Bet* nyumba, mwili, makao. Moyo ni kitu kilicho ndani ya nyumba ya mwili, kikiwa bustani ya ndani. Hivyo moyo unanyuliwa kupitia mlango, kuongozwa katika mamlaka ya uzima. *HISIA NA KUANGUKA* Hisia = kitu kinachonyanyuka kutoka moyoni. Zinaweza kupingana na mkono wa haki na kuinua moyo katika tamaa. ...