AfyaYako | FAIDA NA MAAJABU YA KAROTI KATIKA AFYA MWILINI

 

Bonyeza hapa kutazama Video ili ujue na Ufahamu zaidi Faida nyingi za Karoti

                    LINK YA VIDEOπŸ‘‡πŸ‘‡

πŸ”΅ 《 VIDEO: FAIDA NA MAAJABU YA KAROTI MWILINI 》


FAIDA YA KULA KAROTI KWA AFYA YA MWILI WAKO


Asilimia kubwa tunapenda kutumia karoti katika kuunga katika mboga ya nyama na si kuila karoti kama karoti. wataalamu wanashauri ili uwe na afya bora unatakiwa ule karoti sita kwa wiki au moja kwa siku. Unaweza kula karoti ya kuchemshaa,juisi au mbichi


Faida ya kula karoti ni kama zifuatazo


i. Karoti husaidia kuimarisha macho kuona vizuri, mfano tatizo la kutoona vizuri usiku, pia inasaidia kuondoa matatizo ya allergy kwenye macho mfano macho kuwasha sababu ya vumbi.


Karoti inarutubisha cells mwilini na kuzifanya zisizeeke haraka. Hii inatokana na uwepo wa Vitamin A ambayo ni muhimu katika kuimarisha uwezo wa macho kuona.


ii. Huifanya ngozi iwe nzui na yenye afya, kama utatumia kurutubisha ngozi yako, ikwangue kwa kutumia grater kiasi unachotaka tia asali mbichi kijiko 1 kikubwa (cha kulia chakula) mafuta ya nzai au olive kijiko kimoja kikubwa na limao kijiko 1 kikubwa changanya vizuri, kisha itumie kusugua mwilini sehemu yoyote unayotaka, ukimaliza acha kama dakika 15 na zaidi kisha oga, itasaidia kuondoa taka katika vinyweleo, kuifanya ngozi iwe laini na kuondoa mikunjo katika ngozi, Kumbuka inatakiwa asali mbichi na siyo asali yoyote.


Karoti husaidia kuondoa sumu na taka mwilini, inaondoa mafuta yasiyotakiwa katika ini (cholesterol) na kuliwezesha lifanye kazi vizui, Kusafisha njia ya haja kubwa na kusaidia kupata choo vizuri (kuzuia constipation).


iii. Karoti zinasaidia kufanya fizi na meno kuwa imara na kuchochea uzalishwaji wa mate.


Pia inasaidia kuzuia stroke (kiharusi, baadhi ya watafiti kutoka vyuo vikuu duniani wanasema ulaji wa karoti sita kwa wiki husaidia kutopata stroke.


Pia wamegundua kaoti zinatibu tatizo la kupoteza kumbukumbu kwa wazee.


iv. Karoti hupunguza hatari ya kupata Shinikizo la Damu (blood pressure) kwani ulaji wa karoti husaidia mwili kupata madini muhimu ya Potassium ambayo husaidia kutanua mirija ya damu (bllod vessels na kufanya damu kufika katika maeneo husika ya mwili (organs).


v. Karoti pia husasidia kuzuia magonjwa mengine kama vile kisukari (Diabetes), Kiharusi (Stroke), Kansa pamoja na magonjwa ya moyo.


vi. Karoti husaidia kuongeza kinga mwilini (immune booster). Kwasababu tabaia asilia ya karoti kuwa na antibacteia pamoja na antiseptic ambazo husaidia kuzuia kinga za mwili. Pia Karoti ina Vitamin C muhimu kwa kusisimua seli nyeupe za damu (white blood cells) ambazo ni sehemu muhimu katika kinga ya mwili.



FAIDA HIZI ZA KAROTI ZITAKUSHANGAZA


Karoti ina faida nyingi sana kwani ina virutubisho vingi muhimu na vinavyohitajika kwa wingi kwenye mwili wa mwanadamu. Karoti ina madini chuma, magnesium, phosphorus, vitamin A, B, C na K, zinc pamoja na calcium.




✍ Karoti hutibu matatizo ya macho na kuboresha afya ya macho

✍ Karoti ni msaada kwa watu wenye Anaemia, huimarisha afya ya watu wenye kisukari na huondoa uchovu wa mwili

✍ Karoti hufanya ngozi kuwa na mvuto, hung'arisha ngozi, huondoa makunyazi, mabaka na kutibu vidonda juu ya ngozi kwa haraka

✍ Karoti hulinda afya ya moyo na kuepusha na athari za saratani

✍ Karoti ni msaada kwa wenye choo kigumu na hupandisha kinga ya mwili

✍ Karoti husaidia mmeng'enyo wa chakula tumboni na husaidia sana kwenye kusafisha mwili

✍ Husaidia kudhibiti kiwango cha sukari katika damu na kukinga na kiharusi

✍ Karoti hulinda ini lisiathiriwe na magonjwa pamoja na kusaidia mwili usichoke mapema na kuzeeka haraka



MUHIMU:

✊ Osha karoti vizuri kabla ya kuzitumia

✊ Unaweza kula karoti kwa kuitafuna yenyewe, kutengeneza juisi yake (usichanganye na sukari) ama kuipika kawaida kwenye mboga

✊ Usile karoti katikati ya mlo ni vyema ikaliwa angalau lisaa limoja kabla na baada ya kula

✊ Kupata faida nyingi za karoti punguza matumizi ya chumvi nyingi, sukari nyingi, vyakula vyenye kemikali na mafuta mengi 

✊ Matumizi ya karoti kwa wingi huweza kubadilisha ngozi kwa 100% hii inaweza kupelekea ngozi kuanza kufanana na karoti 😁


SHARE NA WENZIO WAJIFUNZE KAMA WEWE ↪️

«» Endelea Kufatilia ☆Ng'e Amazing TV kwa Habari, Elimu,  pamoja na Burudani , bonyeza neno SUBSCRIBE pale kwa YouTube channel ili usipitwe na chochote



Comments

Popular posts from this blog

FAHAMU FAIDA ZA KULA DAGAA KWA AFYA

JINSI YA KUPIKA SAMBUSA TAMU ZA VIAZI